DC KINONDONI: “JIAJIRI USISUBIRI KUAJIRIWA”

DC KINONDONI: “JIAJIRI USISUBIRI KUAJIRIWA”

Like
590
0
Wednesday, 03 August 2016
Slider

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi ametambulisha mradi mpya unaoenda kwa jina la ‘JIAJIRI USISUBIRI KUAJIRIWA’ mapema leo katika kipindi cha #JotoLaAsubuhi.

WhatsApp Image 2016-08-03 at 09.47.50

Hapi amesema lengo la mradi huo ni kuwapatia  vijana mitaji inayotokana na vyanzo vya mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni ni sawa na asilimia 10 ya mapato yote yanayopatikana kwa mwaka mzima ambayo hutengwa kwa ajili ya Vijana na Wanawake.

Amebainisha kuwa fedha nyingine wanategemea kuzipata toka kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake ya Milioni 50 kwa kila mtaa. Mradi huo umeanza agosti mosi mwaka huu kwa kutoa fomu kuanzia ngazi ya mtaa ambazo mwisho wa uandikishaji ni agosti nane.

Hapi ameongeza kuwa Serikali au Taasisi nyengine binafsi hazina uwezo wa kuwaajiri watu wote, hivyo serikali inatengeneza mazingira rafiki ili watu wenye sifa za kuajiriwa waajiriwe, na wasiokuwa na sifa waweze kujiajiri wenyewe.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akisilimiana na Mhariri Mkuu wa E-fm Bi Scolastica Mazula.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akisilimiana na Mhariri Mkuu wa E-fm Scholastica Mazula.

Hapi amesema, “Vijana wa Kinondoni wenye nia ya kujiajiri wajitokeze, tumeandaa wakufunzi wa kuwapatia elimu ya ujasiriamali bure. Ifike wakati Vijana waache utaratibu wa kuzunguuka na makaratasi (CV) tuanze kutumia fursa zilizopo. Waachane na kucheza ‘Pool table, kutumia dawa za kulevya na kukaa mtaani bila shughuli zozote. Hapi katika kujibu swali la Gerald Hando alisema “Wakati wa kutoa mitaji hatutatoa kwa mtu mmoja mmoja, tunaomba waunde makundi ili iwe rahisi kuwapatia mitaji hiyo,  Watu wengi wanapenda kupata mikopo toka taasisi za fedha lakini hawana uelewa wakujua ni vipi inapatikana. hii ni changamoto,”

 

Picha ya Paoja na Mkuu wa Wilaya

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akiwa na timu nzima ya Joto la Asubuhi.

 

 

Comments are closed.