DEBI YA MANCHESTER YATIBUKA

DEBI YA MANCHESTER YATIBUKA

Like
302
0
Monday, 25 July 2016
Slider

Mechi ya kirafiki kati ya miamba wa Uingereza, Manchester City na Manchester United, imefutiliwa mbali kutokana na mvua kubwa.

Mechi hiyo ilikuwa imepangiwa kuchezewa uwanja waBirds Nest, Uchina na ingekuwa ya kwanza kwa mameneja wapya Pep Guardiola na Jose Mourinho.

Jumapili, Mourinho alikuwa amedokeza kwamba hali katika uwanja huo ilikuwa mbaya.

Hata kabla ya mechi kuahirishwa rasmi, Guardiola alikuwa amesema matumaini yake ni kwamba wachezaji wake wasiumie.

City na United wamesema “waandalizi wa mchuano huu pamoja na klabu zote mbili” wameamua kuahirisha mechi hiyo iliyopangiwa kuchezewa uwanja uliotumiwa kuandaa michezo ya Olimpiki 2008.

Mvua kubwa ilinyesha Jumapili na watabiri wa hali ya hewa walisema mvua zaidi ingenyesha Jumatatu.

United watarejea Manchester baadaye leo nao City wasafiri hadi Shenzhen Jumanne kwa mechi dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani siku ya Alhamisi.

Comments are closed.