DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA

DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA

Like
455
0
Friday, 16 October 2015
Local News

ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe ambaye alikuwa anatetea nafasi hiyo kupitia chama cha Mapinduzi(CCM), amefariki kwenye ajali ya helikopta iliyotokea jana usiku kwenye hifadhi ya wanyama ya Selous lililopo eneo la Kilombero mkoani Morogoro.

 

Filikunjombe ni mmoja wa abiria watatu waliokuwa ndani ya chopa hiyo ambao imethibitishwa kupoteza maisha.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jerry Silaa, Meya wa Manispaa ya Ilala anayemaliza muda wake, kapteni William Silaa baba mzazi wa Jerry ndiye aliyekuwa rubani wa chopa hiyo ambaye naye amepoteza maisha. Tayari Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo maalumu wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

Comments are closed.