DEREVA WA MASHINDANO YA MAGARI WA AFRIKA KUSINI AFIA TANZANIA NA SIO KENYA

DEREVA WA MASHINDANO YA MAGARI WA AFRIKA KUSINI AFIA TANZANIA NA SIO KENYA

Like
457
0
Tuesday, 19 July 2016
Local News

Bodi ya utalii nchini inakanusha madai ya mwandishi Cara Anna kufuatia taarifa yake aliyoitoa kwenye chombo cha habari cha Miami Herald chenye makao yake nchini Marekani akiripoti kifo cha Gugu Zulu Raia wa Afrika kusini aliyefariki dunia wakati akijaribu kupanda mlima Kilimanjaro, hapa Tanzania.

Kwenye ripoti ya mwandishi huyo amedai kuwa raia huyo wa afrika Kusini amepoteza maisha wakati akijaribu kupanda mlima Kilimanjaro nchini Kenya
Zulu mwenye umri wa miaka 38 ni dereva wa mbio za magari alikuwa katika ziara ya kuchangisha fedha kuenzi juhudi za aliyekuwa Rais wa Afrika kusini Nelson Mandela, kuweza kuwasaidia pia wasichana kuweza kukidhi mahitaji yao maalumu.
Zulu na mkewe Letshego hawakuendelea na safari hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro, baada ya kugundua amepatwa na matatizo ya kupumua.

Awali katika mtandao wa Facebook, alielezea dalili za kusumbuliwa na mafua.

Comments are closed.