DILMA ROUSSEFF ATOA MSIMAMO WAKUTOTISHIKA

DILMA ROUSSEFF ATOA MSIMAMO WAKUTOTISHIKA

Like
193
0
Wednesday, 08 July 2015
Global News

WAKATI tuhuma zikiongezeka juu ya mustakabali wa serikali yake rais Dilma Rousseff  wa Brazil ameliambia gazeti la Folha de Sao Paulo kwamba hatishiki na kwamba hakuna msingi wa yeye kuachishwa kazi na bunge.

Ikiwa ni miezi saba baada ya kuingia katika muhula wake wa pili wa uongozi serikali yake inazidi kutikiswa na kashfa ya rushwa katika kampuni kubwa ya mafuta nchini Petrobras.

Tuhuma za hivi karibuni zinadai kwamba kampeni yake ya kuwania urais ilifadhiliwa kwa fedha haramu kutoka kampuni hiyo huku umaarufu wa Rousseff ukiendelea kupungua kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

 

Comments are closed.