DK BILAL AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA CELINA KOMBANI

DK BILAL AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA CELINA KOMBANI

Like
268
0
Monday, 28 September 2015
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Muhammed Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani aliyefariki Septemba 24 katika hospitali ya Andraprash Apolo Nchini India kutokana na ugonjwa wa Saratani ya Kongosho.

 

Tukio hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali kutoka Tanzania bara na visiwani wakiwemo Mawaziri.

Comments are closed.