DK. BILALI AWATAKA WATAALAMU WA SHERIA KUSAIDIA WATANZANIA WA HALI YA CHINI

DK. BILALI AWATAKA WATAALAMU WA SHERIA KUSAIDIA WATANZANIA WA HALI YA CHINI

Like
272
0
Monday, 22 December 2014
Local News

MAKAMU wa Rais Dokta MUHAMMED GHARIB BILALI amewataka Wataalamu wa Sheria katika taasisi ya mafunzo ya Sheria kwa vitendo nchini kusaidia kutoa huduma za msaada wa Kisheria kwa Watanzania wa hali ya chini wasioweza kumudu gharama za huduma hiyo ili kuongeza chachu ya haki kutendeka.

Dokta BILAL ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa vitendo ambapo amewataka wahitimu wa taasisi hiyo kuutumia Weledi wao katika kusimamia haki nchini ili kuifanya Taasisi hiyo kuwa ni mfano wa kuigwa kwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki.

 

Comments are closed.