DK KIGWANGALLA ATUMBUA MAJIPU YA WACHELEWAJI WIZARA YA AFYA

DK KIGWANGALLA ATUMBUA MAJIPU YA WACHELEWAJI WIZARA YA AFYA

Like
316
0
Friday, 18 December 2015
Local News

NAIBU  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dokta. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini.

 

Awali Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani.

K..

Comments are closed.