DK. SHEIN AONGOZA MAELFU YA WATANZANIA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI

DK. SHEIN AONGOZA MAELFU YA WATANZANIA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI

Like
252
0
Monday, 12 January 2015
Local News

 RAIS WA ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta ALLY MOHAMMED SHEIN leo amewaongoza maelfu ya Watanzania na Viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE katika Maadhimisho ya Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar Dokta SHEIN amezungumzia mafanikio yaliyopatikana nchini humo katika kipindi cha miaka minne ikiwa ni pamoja na Ukuaji wa Uchumi, Ongezeko la Wataalamu wa Afya na kukua kwa kiwango cha elimu.

Comments are closed.