DK SHEIN: NIMETEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM KWA VITENDO

DK SHEIN: NIMETEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM KWA VITENDO

Like
246
0
Wednesday, 16 September 2015
Local News

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amesema kuwa katika uongozi wake ametekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo huku pia, akitekeleza vizuri uongozi wake katika Serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa kwa amani na utulivu.

 

Dk. Shein ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa Kampeni wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.

 

Ametaja baadhi ya mafanikio ya uongozi wake kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 4.5 hadi 7.2  ambapo kwa upande wa pato la taifa limeongezeka hadi trilioni 1.508 kutoka trioni 2.138.

Comments are closed.