DK. SHEIN: TOFAUTI ZA KISIASA ZISIVURUGE AMANI

DK. SHEIN: TOFAUTI ZA KISIASA ZISIVURUGE AMANI

Like
186
0
Thursday, 07 January 2016
Local News

RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta  Ali Mohamed Shein  ametaka tofauti za kisiasa zilizopo Visiwani humo zisitumike kuvuruga amani na utulivu ambayo ndiyo siri kubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika visiwa vya Unguja na Pemba.

 

Dokta Shein ambaye alikuwa akizungumza na wananchi wa Wete waliokwenda kumsalimia mara baada ya kukagua ujenzi wa soko na Ofisi ya Baraza la Mji wa Wete, amesema kuwa suala la amani halina mbadala huku akiahidi kuendelea kuisimamia amani ya Zanzibar na kusikitishwa na wale wote wanaotaka kuvuruga amani kwa kisingizio cha kuiongoza Zanzibar

Comments are closed.