DKT. SHEIN: ZANZIBAR HAPATAKUWA NA UCHAGUZI HADI MWKA 2020

DKT. SHEIN: ZANZIBAR HAPATAKUWA NA UCHAGUZI HADI MWKA 2020

Like
303
0
Tuesday, 31 May 2016
Local News

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amewaeleza wananchi kisiwani Pemba kuwa Zanzibar hapatakuwa tena na uchaguzi hadi mwaka 2020 na kwamba kwa sasa yeye ndiye Rais aliyechaguliwa kihalali na wananchi.

Dokta Shein ameyasema hayo huko Tibirinzi Chake Chake Pemba, alipokwenda kukagua Tawi la CCM lililochomwa moto katika ziara yake ya kukagua athari zilizofanywa dhidi ya Wana CCM kwa kuendelea kukiunga mkono chama hicho kiswani humo.

Mbali na hayo amewataka wananchi kuyapuuza maneno ya utani na dhihaka wanayoambiwa wananchi kuwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar utarudiwa tena na kusema kuwa hilo halipo na hakuna hata taifa au nchi inayoweza kuishurutisha Zanzibar kufanya uchaguzi.

Comments are closed.