ASILIMIA 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA) yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.
Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.
Profesa Manyele aliongeza kuwa mikoa ya kanda ya Ziwa, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya ndio inayoongoza kwa matokeo ya uchanguzi huo wa makosa ya Vinasaba nchini.