DOKTA MAKONGORO MAHANGA ASIKITISHWA NA TAARIFA YA KUZUSHIWA KIFO

DOKTA MAKONGORO MAHANGA ASIKITISHWA NA TAARIFA YA KUZUSHIWA KIFO

Like
328
0
Monday, 23 May 2016
Local News

ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana,katika serikali ya awamu ya nne, Dokta  Makongoro Mahanga, amesema amesikitishwa na uvumi wa taarifa kuwa amefariki dunia.

Akizungumza kwa njia ya simu na Efm Habari, Dokta Mahanga amesema hata yeye hajui ni nani ametoa taarifa hizo ambazo siyo za kweli na amewaomba watanzania kuitumia vyema mitandao badala ya kuibuka na taarifa ambazo hazina uhakika.

Comments are closed.