Dola 250,00 Kulala Gereza Alimofungwa Mandela

Dola 250,00 Kulala Gereza Alimofungwa Mandela

1
556
0
Thursday, 05 July 2018
Global News

Mnada unafanyika nchini Afrika Kusini wa kutoa fursa kwa watu kuweza kulala kwa siku moja kwenye jela alimofungwa rais wa kwanza mweusi nchini humo Nelson Mandela huko Robben Island.

Shirika moja linafanya mnada huo wa kuanzia dola 250,000 kuruhusu watu 67 kulala kwa siku moja ndani ya gereza la ulinzi mkali ambapo Mandela alifungwa kwa miaka 18 kati ya miaka 27 ya kifungo chake.

Warsha hiyo inaandaliwa na kundi linalofahamika kama CEO Sleepout, kuadhimisha siku ambayo Mandela ambaye alifariki mwaka 2013 akiwa na miaka 95 angefikisha miaka 100.

Linasema kuwa mnada huo utafungwa usiku wa manane tarehe 17 Julai siku moja kabla ya kuadhimishwa siku yake ya kuzaliwa.

Warsha hiyo inaandaliwa na kundi linalofahamika kama CEO Sleepout, kuadhimisha siku ambayo Mandela ambaye alifariki mwaka 2013 akiwa na miaka 95 angefikisha miaka 100.

Linasema kuwa mnada huo utafungwa usiku wa manane tarehe 17 Julai siku moja kabla ya kuadhimishwa siku yake ya kuzaliwa.

Mandela aliachiliwa kutoka gerezani mwaka 1990 wakati Afrika Kusini ulikuwa unaupigia kwaheri ubaguzi wa rangi, jambo lililofikia kikomo mwaka 1994 wakati alichaguliwa kama rais wa kwanza mweusi nchini humo.

Baadhi ya pesa ambazo zitapatikana kutoka kwa mnada huo zitapewa kundi moja la kimarekani linalowasaidia wafungwa kupata elimu cha chuo kikuu.

“Nilienda likizo ndefu ya miaka 27,” Nelson Mandela wakati mmoja alisema kuhusu miaka yake gerezani.

Maneno kwanza ya mlinzi wa gereza wakati Nelson Mandela na wenzake wa ANC walifika yalikuwa ni: “Hiki ni kisiwa, Hapa ndipo mtafia.”

Walipitia maisha mabaya kwenye gereza hilo jipya lililojengwa kuwazuia wafungwa wa kisissa. Kila mmoja alikuwa na chumba chake ya futi saba mraba na kilizungukwa na ua uliojengwa waka saruji. Kwanza hakuruhusiwa kusoma chochote.

Walivunja mawe kwa nyundo kutengeneza kokoto na walilazimishwa kufanya kazi kwa timbo lililokuwa na mwangaza mkali.

Mfungwa mwenzake Walter Sisulu alingumza kuhunu kuibuka kwa uongozi wa Mandela miongoni mwa wafungwa kauanzia uasi kwenye matimbo.

Mfungwa nambari 46664 jinsi alivyofahamika – mfungwa wa 466 kuwasili mwaka 1964 – akawa wa kwanza kuasi kupinga kutendewa vibaya na mara nyingine alitenganishwa na wafungwa wengine kama adhabu.

Wakati wa miaka ya kwanza kwanza, kutengwa ilikuwa kawaida. Tulihukuiwa kwa makosa madogo na kutengwa, aliandika kwenye kitabu chake, The Long Walk to Freedom. Mamlaka ziliamini kuwa kutengwa ilikuwa jibu kwa uasi wetu.

Baada ya miezi michache ya kwanza kwenye kisiwa cha Roben, maisha yalirudi kuwa ya mpangilio.

“Maisha ya gerezani na mpangilio: kila siku ni sawa na iliyopita, kila wiki ni sawa na iliyotangulia na hivyo miezi na miaka huingiliana, Mandela aliandika.

Muda ulivyopita na kulingana ni alikuwa akisimamia gereza, mambo kadhaa yaliruhusiwa. Wale waliotaka walituma maombi ya kusoma.

Lakini masomo mengine kama ya siasa na historia ya jeshi vilikuwa haramu. Robben Island ikaja kufahamika kama “chuo ndani ya gereza.”

Wakati Mandela alizungunzia maisha yake huko Robben baada ya kurudi huko mwaka 1994 alisema: “Vidonda ambavyo havionekani, ni vichungu sana kuliko vile vinavyoweza kuonekana na kutibiwa na daktari. Moja ya nyakati zenye husuni zaidi wakati wa miaka yangu gerezani ulikuwa wakati wa kifo cha mama yangu. Wakati mwingine ni wakati wa kifo cha mtota wangu wa kwanza wa kiume aliyefariki kwenye ajali ya barabarani.” hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi yote hayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *