DONALD TRUMP ASHTUMIWA VIKALI KWA KUPANGA KUTIMUA WAHAMIAJI

DONALD TRUMP ASHTUMIWA VIKALI KWA KUPANGA KUTIMUA WAHAMIAJI

Like
184
0
Wednesday, 11 November 2015
Global News

DONALD TRUMP, mmoja wa wanaowania nafasi ya Urais kupitia chama cha Republican katika Uchaguzi mkuu nchini Marekani, ameshutumiwa vikali kutokana na mpango wake wa kuwafukuza wahamiaji milioni 11 kutoka nchini humo.

Kwenye mdahalo wa moja kwa moja kupitia runinga, wagombea wengine wawili wanaoshindana naye, John Kasich na Jeb Bush, waliukosoa vikali mpango huo wakisema hauwezi kutekelezeka na ni kitendo cha ubaguzi.

Hali hiyo imesababisha watu waliohudhuria mdahalo huo kumzomea Trump, wakati alipojaribu kujitetea kuhusu huo mpango wake.

Comments are closed.