Donald Trump hatousikiliza mkanda wa sauti ya mauwaji ya Khashoggi

Donald Trump hatousikiliza mkanda wa sauti ya mauwaji ya Khashoggi

Like
488
0
Monday, 19 November 2018
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amejuzwa kuhusu mkanda wa sauti wa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi lakini amesema binafsi hatousikiliza.
“Ni mkanda wa maumivu, ni mkanda mbaya,” Trump ameiambia runinga ya Fox News.
Shirika la ujasusi la Marekani CIA linaaminika kufikia kikomo kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman aliamrisha kutekelezwa kwa maujai hayo, japo bado Ikulu ya White House haijathibitisha uchunguzi huo.
Saudi Arabia imeziita taarifa hizo kuwa ni za uongo na kudai kuwa bin Salman hakuwa na taarifa yoyote juu ya kutekelezwa kwa mkasa huo.
Khashoggi, alikuwa ni kinara wa kuukosoa utawala wa kifalme wa Saudia. Aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul Oktoba 2 alipoenda kuchukua karatasi zake za talaka.
Saudia inasema aliuawa katika operesheni haramu iliyotekelezwa na maafisa wake wa usalama.
Hata wanaomuunga mkono Trump ndani ya Bunge la Wawakilishi wanamtaka achukue hatua kali juu ya mauaji hayo. Lakini kutokana na unyeti wa Saudia kama mshirika thabiti wa Marekani katika Mashariki ya Kati kunamfanya Trump kuwa mgumu katika kufanya maamuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *