Katika ligi kuu ya England mechi 12 zimechezwa usiku wa kuamkia leo ambapo Tottenham wamewabamiza bila huruma Asteras Tripolis kwa magoli 5 -1.
Ilikuwa ni hat-trick ya Harry Kane ambayo imeisaidia Tottenham kuwabamiza wagiriki hao.
Wakati Evarton imewatunishia misuli Wafaransa, Mpaka dakika ya 90, si Lilli wala Everton aliyechezea nyavu za mwenzie.
Mchezo huo uliotanguliwa na mapambano kati ya Polisi na Mashabiki wa Evarton ukaisha bila bila.
Divock Okoth Origi mchezaji kinda ameonyesha mchezo mzuri katika mechi hiyo, Divock aliyezaliwa mwaka 1995 ni mtoto wa
aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Kenya na Mchezaji wa kulipwa Mike Origi.
Hata hivyo kijana huyo ni binamu wa Arnold Origi, Mkenya anayesukuma ngozi ya ngombe huko Norway.
Matoke mengine ni Villarreal imemchapa FC Zürich mabao 4 – 1. Hapo Kesho Jumamosi, West Ham wanapambana na Man City,
Liverpool watakuwa uso kwa uso na Hull, Southampton kutoana jasho na Stoke, Sunderland jumamosi iliyopita walipigwa bao 8
kiasi wakaamua kuwarudishia kiingilio mashabiki wao, je! watapona mbele ya bunduki za Arsenal.