DRC: MASHIRIKA YA KIRAIA YAMEIOMBA UN KUFIKIRIA UPYA MPANGO WA KUJIONDOA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA FDLR

DRC: MASHIRIKA YA KIRAIA YAMEIOMBA UN KUFIKIRIA UPYA MPANGO WA KUJIONDOA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA FDLR

Like
201
0
Thursday, 12 February 2015
Global News

MASHIRIKA mbali mbali ya kiraia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameomba majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo MUNUSCO kufikiria upya mpango wake kujiondoa kupambana na kundi la waasi la FDLR.

Hapo jana majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo yalitangaza kujiondoa katika operesheni hiyo kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya DRC hadi hapo serikali ya Kongo itakapotengua uteuzi wa majenerali wawili walioteuliwa kuongoza opereshini hiyo.

Kwa mujibu wa MUNUSCO majenerali hao wana tuhumiwa kufanya vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

 

Comments are closed.