DRC: WANAHARAKATI WAMEZIONYA SHULE KUTOSAJILI WATOTO JESHINI

DRC: WANAHARAKATI WAMEZIONYA SHULE KUTOSAJILI WATOTO JESHINI

Like
265
0
Wednesday, 28 October 2015
Global News

WANAHARAKATI wa kutetea Haki za Binadamu wamezionya shule za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC, kutowaandikisha watoto wa shule hizo kujiunga jeshini.

Kundi la wanaharakati hao lenye makao yake makuu nchini Marekani limesema kuwa makundi yenye silaha yamekuwa yakiwateka wanafunzi katika majimbo ya Kivu ya kaskazini na kusini na kuwalazimisha kujiunga na Jeshi.

Katika ripoti yake, kundi hilo pia limeyalaumu makundi ya waasi na jeshi la serikali ya Congo, kwa kutumia shule kama kambi zake za kijeshi au kuhifadhia silaha.

Comments are closed.