DUKA LA DAWA LA MSD LAZINDULIWA MWANZA

DUKA LA DAWA LA MSD LAZINDULIWA MWANZA

Like
470
0
Friday, 22 January 2016
Local News

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mheshimiwa Ummy Mwalimu amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo lipo ndani ya Hospitali ya SekouToure, na kufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dkt John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana.

 

Katika hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, Waziri Ummy ameipongeza MSD kwa hatua hiyo nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na kuitaka MSD kukamilisha ufunguzi wa maduka mengine mawili yaliyosalia katika mikoa ya Arusha naMbeya.

 

Mbali na hayo ameeleza kuwa Wizara yake imejiwekea malengo ya upatikanaji wa dawa nchini kutoka asilimia 70 kwa sasana kufika hadi asilimia 95.

UMMY2

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Ummy Mwalimu (kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza jana ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD, Profesa Idrisa Mtulia.

Comments are closed.