DUNIA YAADHIMISHA SIKU YA FIGO LEO

DUNIA YAADHIMISHA SIKU YA FIGO LEO

Like
340
0
Thursday, 10 March 2016
Local News

WATANZANIA leo wanaungana na watu wote duniani kuadhimisha siku ya Figo na tafiti za ugonjwa huo zinaonyesha kuwa kati ya mwezi Agosti 2014 na Februari 2015 kati ya watoto 513 waliopimwa magonjwa ya figo katika Hospitali za Bugando na Sekou Toure asilimia 16.2% walikuwa na matatizo ya figo.

 

Siku ya Figo Duniani huadhimishwa duniani kote kila Alhamis ya pili ya mwezi Machi tangu mwaka 2006. Mwaka huu inaadhimishwa leo ikiwa na Kaulimbiu isemayo “Chukua Hatua Mapema Kuepuka Magonjwa ya Figo kwa Watoto”.

 

Wizara Kwa kushirikiana na Chama cha Watalaam wa Magonjwa ya Figo Tanzania imekuwa ikitoa elimu ya kujikinga na madhara ya magonjwa ya figo kwa kuzingatia kanuni za afya na kupima mapema ili kutambua na kupata matibabu kwa wakati.

Comments are closed.