E-FM YAILAZA BOKO BEACH VETERANI 3-1

E-FM YAILAZA BOKO BEACH VETERANI 3-1

Like
575
0
Saturday, 19 December 2015
Slider

E-fm imeufunga mwaka kimichezo kwa kipute cha dakika 90 za mpira wa miguu dhidi ya maveterani wa Boko Beach katika uwanja wa Boko Beach.

E-fm ilifanikiwa kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza na kuweza kuzitandika nyavu za Boko Beach Veterani magoli mawili.

Kasi ya mchezo ilibadilika katika kipindi cha pili baada ya E-fm kuandika bao lake la tatu kupitia nyota wake John Makundi, goli hilo liliamsha kikosi cha Boko Beach Veterani  kwa kuutumia vizuri mpira wa adhabu kwa E-fm kujipatia bao moja lilifungwa na mchezaji wake Kudra Omar, bao liliodumu hadi mwisho wa mchezo efm wakiibuka wababe kwa jumla ya magoli 3-1

1

Picha ya pamoja ya kikosi cha E-fm

2

 

Picha ya pamoja ya kikosi cha cha Boko Beach Veterani

3

Ibrahim Masoud Maestro akiambaa na mpira

 

4

Mlinda mlango wa Boko Beach Veterani akijaribu kuwapanga walinzi wake

5

Nahodha wa Efm Ssebo akitoka nje ya uwanja baada ya kulimwa kadi nyekundu

Comments are closed.