EABC YATOA MAFUNZO KWA WAHANDISI WASANIFU TANZANIA

EABC YATOA MAFUNZO KWA WAHANDISI WASANIFU TANZANIA

Like
302
0
Monday, 03 November 2014
Local News

BARAZA la wafanyabiashara Afrika mashariki –EABC- limetoa mafunzo kwa wahandisi wasanifu kuihamasisha Serikali ya Tanzania iweze kusaini mkataba wa makubaliano ya kutambulika katika nchi tano ili kuwawezesha kupata fursa za biashara na kazi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Tanzania kuwa nchi pekee iliyobakia kusaini makubaliano hayo kutokana na kutokukubaliana na baadhi ya mambo ambayo wana uhakika yanaweza kurekebishwa na kuruhusu mkataba huo kusainiwa.

Akizungumza na EFM mjumbe wa EABC ADRIAN NJAU amesema mpaka sasa wameshasaini makubaliano matatu ambayo yanaruhusu wahasibu,wasanifu na wahandisi wasanifu kutambulika nchi zote jambo linalowaruhusu kufanya kazi katika nchi hizo bila kufanya usajili wowote zaidi ya kuuliza kama mhusika ni mwanachama.

 WAFANYABIASHARA

 AMEONGEZA kuwa lengo kubwa ni kuhamasisha watanzania wenye vigezo kuweza kutumia fursa hiyo kujipatia nafasi za kazi katika nchi hizo za Afrika ambazo ni Rwanda,Uganda,Kenya na Burundi ikiwemo Tanzania.

 

 

Comments are closed.