Nchi ya Cuba imejitolea Madaktari 75 na wauguzi 10 kwenda kusaidia nchi zilizoathirika na maradhi ya ugonjwa wa Ebola Afrika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Balozi wa Cuba nchini Tanzania GEORGE LOPEZ amesema katika kukuza Umoja na Ushirikiano kati ya nchi ya Cuba na Afrika,wameamua kujitolea madaktari hao kusaidia kutoa hudumaza Matibabu katika nchi za Sierion,Liberia.
Balozi LOPEZ amesema nchi yake itazidi kuisadia Afrika hasa katika sekta ya afya na elimu.