EBOLA: IDADI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA SIERRA LEONE, GUINEA NA LIBERIA NI ZAIDI YA 10000

EBOLA: IDADI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA SIERRA LEONE, GUINEA NA LIBERIA NI ZAIDI YA 10000

Like
292
0
Friday, 13 March 2015
Global News

IDADI ya watu waliofariki kutokana na maradhi ya Ebola katika nchi tatu za Afrika magharibi zilizoathirika zaidi na maradhi yao, Guinea, Sierra Leone na Liberia imezidi watu 10,000.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya la Umoja wa mataifa WHO iliyochapishwa mjini Geneva.

Hata hivyo shirika hilo limesema maradhi hayo yamepungua hivi sasa na kuna matukio machache mapya ya Ebola yaliyosajiliwa.

 

Comments are closed.