EBOLA: MAAFISA WA AFYA MAREKANI WATOA MWONGOZO MPYA

EBOLA: MAAFISA WA AFYA MAREKANI WATOA MWONGOZO MPYA

Like
273
0
Tuesday, 28 October 2014
Global News

Maafisa wa afya wa Marekani wametoa mwongozo mpya juu ya kuwashughulikia matabibu wanaorudi Marekani baada ya kuwahudumia wagonjwa wa Ebola Afrika Magharibi.

Mwongozo huo unapendekeza kuwa wanaoshukiwa kuwa katika hatari ya kuwaambukiza wengine watazuiliwa nyumbani kwao; ingawa majimbo tofauti yatakuwa na uhuru wa kutoa mwongozo thabiti zaidi.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amepinga hatua hizo za kuwaweka karantini walioathirika.

EBOLA

Muuguzi Kaci Hickox aliyeonya kwenda mahakamani kwa kutengwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mlipuko wa ugonjwa wa ebola afrika magharibi umewaathiri zaidi ya watu 10,000 na kuwaua takriban watu 5,000.

Tangazo hilo la Marekani linajiri baada ya muuguzi aliyelalama kuhusu kutengwa kwake katika jimbo la New Jersy kutakiwa kurudi nyumbani.

Akikaidi mahitaji hayo mapya ,gavana wa New Jerzy Chris Christie alitetea mahitaji hayo ya karantini aliyowekewa Kaci Hickox wakati alipowasili kutoka Sierra Leone .

Ameongezea kuwa wataendelea kuchukua hatua kama hizo.

Msimamo huo unatofautiana na ule wa katibu mkuu umoja wa mataifa Ban Ki Moon ambaye awali alisema kuwa wale wanaotaka kutoa msaada wasiwekewe vikwazo ambavyo haviambatani na sayansi.

Alisema kwamba wale wamepata maambukizi wanafaa kusaidiwa na sio kutengwa.

Watu walioathirika hawawezi kuambukiza hadi watakapoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

 

 

Comments are closed.