MFUKO wa Bill na Melinda Gates umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7 kwa ajili ya mradi kusaidia matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini Guinea na nchi nyingine zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
Mfuko huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio.
Zaidi ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka Afrika Magharibi.
Hata hivyo kuna chanjo kadhaa za majaribio na dawa za kutibu maradhi ya Ebola, lakini hazijajaribiwa kwa ajili ya kuona usalama wake na namna zinavyofanya kazi. Shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF linatarajia kuanzisha majaribio ya tiba Afrika Magharibi mwezi Desemba.