EBOLA: TAHADHARI YA MAAMBUKIZI ZAIDI YATOLEWA SIERRA LEONE

EBOLA: TAHADHARI YA MAAMBUKIZI ZAIDI YATOLEWA SIERRA LEONE

Like
173
0
Tuesday, 14 July 2015
Global News

MAOFISA wa Afya nchini Sierra Leone wametahadharisha uwezekano wa kutokea kwa maambukizi zaidi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni mwaka mmoja tangu mgonjwa wa kwanza kubainika nchini humo.

Wamesema kuwa hofu ya baadhi ya watu kukataliwa na kutengwa na jamii ni moja ya sababu inayochangia kuenea kwa maambukizi hayo kwani wengi hujificha wanapokumbwa na ugonjwa huo.

Hata hivyo kumekuwa na kasi ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika siku za hivi karibuni ingawa katika makao makuu ya nchi hiyo Freetown kumekuwa na maambukizi mapya ya ugonjwa huo..

Comments are closed.