CHANJO ya ugonjwa wa Ebola imeanza kufanyiwa majaribio nchini Liberia, ambapo wafanyakazi 600 wa kujitolea wanatarajiwa kushiriki katika awamu ya kwanza ya majaribio hayo.
Chanjo hiyo inayolenga kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Ebola, imeanza kutolewa jana kwenye mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Ingawa Waliberia wengi wameonyesha wasiwasi, wataalamu wa afya wamesema chanjo hiyo tayari imeonyesha mafanikio na ni salama kwa matumizi ya binaadamu.