EBOLA YATINGA TANZANIA!!!

EBOLA YATINGA TANZANIA!!!

Like
543
0
Monday, 20 October 2014
Local News

 

MWILI wa mtu mmoja anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola Wilayani Sengerema Mkoani mwanza umezikwa jana kwa tahadhari kubwa na wataalamu wa afya.

Mgonjwa huyo anayedaiwa kufariki kwa Ebola Salome Richard mwenye umri wa miaka 17, alifikishwa katika hospitali ya Sengerema siku ya Ijumaa wiki iliyopita nakufariki siku hiyo hiyo.

Kwa mujibu wa muunguzi aliyempokea mgonjwa huyo SUZANA JONATHAN ambaye pia bado amewekwa chini ya uangalizi maalumu, mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo akiwa anatokwa damu sehemu mbalimbali za wazi mwilini, amevimba, haoni lakini pia alikuwa anatapika na homa kali.

Comments are closed.