EFM NA DTB BANK KUADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUFANYA USAFI

EFM NA DTB BANK KUADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUFANYA USAFI

Like
327
0
Monday, 07 December 2015
Local News

EFM Radio kwa kushirikiana na  Benki ya DTB na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Paul Makonda, tumeamua kuunga mkono na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli la kuadhimisha Siku ya Uhuru 09/12/ 2015 kwa kufanya Usafi: ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuondoa ama kumaliza kabisa tatizo la magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.

 

EFM na DTB Bank, tutashirikiana na  wakazi wa Mji huu wa Dar es salaam wakiwemo wasanii mbalimbali lakini tukiongozwa pia na Viongozi mbalimbali wastaafu na walioko madarakani ,  Siku hiyo tumeipa kauli mbiu isemayo “naona aibu  kuishi na Uchafu”, tukiunga mkono kauli mbiu  ya Wilaya ya Kinondoni inayosema  Naona aibu kuichafua Kinondoni  “USAFI  UANZE NA MIMI”

Maeneo ambayo tunatarajia kuyafanyia usafi ni barabara inayoanzia  Moroco kuelekea Magomeni.

 

Hivyo basi, tunaomba pia kutumia nafasi hii kuwaomba wateja wote wa DTB Bank ,  wasikilizaji wa EFM  pamoja na wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kuungana nasi siku hiyo ya Uhuru kwa Usafi wa mazingira ya nchi yetu. HAPA KAZI TU.

DSC_0174

DSC_0137

Comments are closed.