EFM REDIO YATIMIZA MWAKA MMOJA KWA KISHINDO

EFM REDIO YATIMIZA MWAKA MMOJA KWA KISHINDO

Like
1123
0
Thursday, 02 April 2015
Local News

WATANZANIA wameaswa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae pamoja na kuliletea Taifa maendeleo.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM,FRANCIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za urushaji wa matangazo ya Efm Radio.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meya wa Manispaa ya Kinondoni YUSUPH MWENDA, Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa DAVID KAFULILA, Mheshimiwa ZITTO KABWE na Mkurugenzi wa Masoko kutoka Zantel, SUKHWINDER BAJWA.

Katika hafla hiyo SIZA amesema kuwa ni muda muafaka sasa kwa Watanzania kubadili maisha yao kuwa chanya kupitia E FM na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano, kwani E FM ipo kw aajili ya Watanzania.

Wakati huohuo,Mstahiki Meya wa MANISPAA ya Kinondoni YUSUPH MWENDA amesema kuwa, mbali na Efm kutoa Burudani pia imetoa mchango mkubwa kutatua changamoto kwa wananchi.

MWENDA amewasihi wananchi hususani wa Kinondoni kutumia vyema matangazo ya Efm Radio ili iwe rahisi kutatua kero mbalimbali.

Naye Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa DAVID KAFULILA amesema kuwa, ameguswa kwa kiasi kikubwa na vipindi mbalimbali vinavyoendeshwa na Kituo hiki kwa kuwa vinaligusa Taifa.

Akimzungumzia kumkumbuka ZITTO KABWE akiwa ni rafiki yake Bungeni na ni mmoja ya Wabunge wanaotoka wote mkoani wa Kigoma,  Mheshimiwa KAFULILA amesema kuwa ,ZITTO alikuwa ni miongoni mwa Wabunge vijana walioleta mabadiliko makubwa ya Kisiasa nchini.

Kwa upande wake Mheshimiwa ZITTO KABWE amesema, kwa kipindi kifupi,  EFM imeonesha Taswira ya hali ya juu inayoakisi hali halisi ya chombo cha habari kinavyotakiwa kuwa.

ZITTO amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kituo hiki kimeonesha utofauti na Vyombo vya Habari vingine kwa kuwa kinajali sauti za Wanyonge na si watu wenye nyadhifa Fulani katika jamii.

1

EFM’s birthday cake.

 

 

 

 

 

 

 

 

2

Mstahiki Meya wa Kinondoni akibadilishana mawazo na Muheshimiwa David Kafulila walipo kutana katika ofisi za EFM asubuhi ya leo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

4

Bwana Sukhwinder Bajwa,yeye ni mkuu wa masoko kutoka kampuni ya Zantel.Alikuja kuipongeza EFM siku ya leo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

5

Samira Kiango ambae ni Mhariri Msaidizi pamoja na Mkurugenzi mkuu wa EFM Bwana Francis Ciza.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

6

Muheshimiwa David Kafulila alipokua akiongea moja kwa moja kutoka katika kituo cha 93.7 EFM siku ya leo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

7

Tulikata keki kwa pamoja.

 

 

 

 

 

 

 

 

8

Jeneral meneja wa EFM Geofrey Ndaula,alikipiga stori mbili tatu na Reuben Ndege(Ncha kali)pamoja Sostenas Ambakisye(Rdj-Kamokali).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

10

Picha ya familia yetu.

 

 

 

 

 

 

 

 

11

Happy birthday EFM.

 

 

 

 

 

 

 

 

14

Samira Kiango pamoja Muheshimiwa David Kafulila.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments are closed.