EFM YATIMIZA MWAKA MMOJA

EFM YATIMIZA MWAKA MMOJA

Like
400
0
Thursday, 02 April 2015
Local News

WATANZANIA wameaswa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae pamoja na kuliletea Taifa maendeleo.
Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM -FRANSIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za Urushaji wa Matangazo wa Kituo hiki ambapo pia imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo meya wa Manispaa ya Kinondoni,YUSUPH MWENDA na Mbunge wa Kigoma Kusini mheshimiwa DAVID KAFULILA,ZITTO KABWE na Mkurugenzi wa masoko wa zantel SUKHWINDER BAJWA
Katika hafla hiyo SIZA amesema kuwa ni muda muafaka sasa kwa watanzania kubadili maisha yao kuwa chanya kupitia E FM kwa kushiriki masuala yote muhimu yanayoanzishwa na kuendelezwa na kituo hiki.

Comments are closed.