EPL: LEICESTER CITY YANYEMELEA UBINGWA!!!

EPL: LEICESTER CITY YANYEMELEA UBINGWA!!!

Like
271
0
Monday, 02 May 2016
Slider

Leicester City wamebakiwa na alama mbili pekee kuupata ushindi wa ligi kuu ya England baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki katika dimba la Stamford Bridge.

Mbweha walipata afueni baada ya kuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa na Antony Martial dakika ya nane ya mchezo kabla ya kusawazisha na kepten Wes Morgan dakika ya 17. Pande zote mbili zilinyimwa mikwaju ya penalti baada ya mlinzi Marcos Rojo kumzuia Riyad Mahrez ndani ya eneo la 18 huku pia Danny Drinkwater wa Leicester akimvuta Memphis Depay ndani ya eneo la hatari.

kwa matokeo hayo Leicester wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi ya England wakiwa na alama 77. Claudio Ranieri huyo akisisitiza kuwa hawakufuata kikombe OT bali kucheza mchezo safi lakini Man U walikua wazuri zaidi yao. Matokeo mengine Liverpool walikiona cha mtema kuni baada ya kuchapwa 3-1 walipokuwa wageni wa Swansea huku Man city wakiambulia kichapo cha mbwa mwizi 4-2 walipowatembelea Sauthampton.

Comments are closed.