MBUNGE wa Bariadi Magharibi kupitia chama cha Mapinduzi -CCM, Andrew Chenge amepandishwa kizimbani kwa madai ya kukiuka maadili ya viongozi wa umma, chini ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili lililoketi, jijini Dar es Saalam asubuhi ya leo.
Katika shauri linalomkabili Chenge ni dhidi ya kukiuka vifungu hivyo vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma, ambapo ilielezwa kuwa, Miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ni pamoja na alipokuwa Mtumishi mkuu wa serikali kwa wadhifa wa mwanasheria Mkuu wa Serikali AG, alipitisha mikataba mbaalimbali dhidi ya IPTL, na baadae alipostaafu nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu alikuwa miongoni mwa Washauri wakuu wa kampuni ya V.I.P Engineer.
Imeelezwa kuwa, Chenge hakuwahi kueleza tume hiyo ya Maadili kama ana madai ama ana hisa na kampuni hiyo ya V.I.P ambayo iliingia ubia na IPTL Katika uuzwaji wa hisa hali ambayo moja kwa moja ilipelekea kukiuka vifungu vya sheria.