ESCROW: KUJIUZULU KWA PROF. MUHONGO HAITOSHI

ESCROW: KUJIUZULU KWA PROF. MUHONGO HAITOSHI

Like
265
0
Thursday, 29 January 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa pamoja na kijiuzulu kwa Profesa Sospeter Muhongo, bado hatua hiyo haitoshi kutatua tatizo la wizi mzito wa fedha za umma kwakuwa wahusika wakuu wa uchotaji wa fedha hizo, bado hawajakamatwa na hata kuhojiwa na hivyo mjadala wa Escrow bado ungali mbichi.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa CHADEMA Arcado Ntagazwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliojadili namna sakata la Tegeta Escrow linavyoendeshwa.

Akifafanua hayo Ntagazwa amesema kuwa hatua madhubuti za kushughulikia ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazijakamilika na haziwezi kukamilika bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa Gavana wa benki kuu, Waziri wa fedha na katibu wake pamoja na maofisa wa Ikulu na Rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.

 

Comments are closed.