ESCROW: SHIRIKISHO LA WANAFUNZI ELIM YA JUU LAMPONGEZA JK

ESCROW: SHIRIKISHO LA WANAFUNZI ELIM YA JUU LAMPONGEZA JK

Like
432
0
Wednesday, 24 December 2014
Local News

SHIRIKISHO la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini limempongeza Rais JAKAYA KIKWETE kwa hotuba nzuri maamuzi sahihi aliyoyachukuwa dhidi ya watuhumiwa wa ukwapuaji wa mabilioni ya pesa kupitia akaunti ya Tegeta Escrow.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho hilo CHRISTOPHER NGUBIAGAI amesema Hotuba ya Rais pamoja na maamuzi yake vimelenga kuamsha fikra kwa vijana na wasomi kutambua maadili ya viongozi na nini kiongozi anapaswa kufanya kwa jamii.

NGUBIAGAI amesema Rais KIKWETE hakumuonea mtu katika maamuzi ndani ya hotuba yake bali amefanya maamuzi sahihi yaliotarajiwa na wengi wana hakumung’unya maneno ili kuhakikisha analinda miiko ya uongozi na watumishi wa umma katika kuitumikia jamii.

Aidha NGUBIAGAI amesema shirikisho limekusudia kuanzisha vipindi katika Radio na TV ili kufanya uchambuzi wa hotuba ya Rais na kutoa ufafanuzi juu ya maamuzi ya Rais katika sakata la ESCROW.

 

Comments are closed.