UPIGAJI kura umesogezwa hadi leo Jumatatu katika baadhi ya maeneo nchini Ethiopia, ili kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki katika uchaguzi mkuu ambao chama tawala kinatazamiwa kushinda kwa kishindo na kuendeleza utawala wake.
Jana Jumapili, wapigakura wa upinzani walidai kuwepo na unyanyasaji na hata vurugu katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.
Karibu asilimia 80 ya wapigakura milioni 35 wa Ethiopia walijiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ambao wengi wanahisi matokoea yake tayari yanajulikana, katika taifa ambako chama tawala kina viti 546 kati ya jumla ya viti 547 vya ubunge.