ETHIOPIA YAOMBOLEZA VIFO VYA RAIA WAKE WALIOUAWA NA IS

ETHIOPIA YAOMBOLEZA VIFO VYA RAIA WAKE WALIOUAWA NA IS

Like
217
0
Tuesday, 21 April 2015
Global News

ETHIOPIA imeanza siku tatu za maombolezi ya Kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na Wanamgambo wa kundi la Islamic State nchini Libya.

Bendera zitapepea nusu mlingoti wakati pia bunge la nchi hiyo litakutana kujadili hatua ambazo litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi ya Ishirini.

Msemaji wa serikali REDWAN HUSSEIN, amesema kuwa waathiriwa hao wanaaminika kuwa wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani ulaya.

Comments are closed.