ETHIOPIA YAONYWA KUKUMBWA NA BALAA LA NJAA

ETHIOPIA YAONYWA KUKUMBWA NA BALAA LA NJAA

Like
275
0
Tuesday, 08 December 2015
Global News

SERIKALI ya Ethiopia imeonya kuwa watu milioni 10 wanakabiliwa na janga la njaa kufuatia ukame mkubwa uliokumba maeneo mengi nchini humo.

Ukame huo umekadiriwa kwamba utaathiri takriban watoto milioni 6 ambao watahitaji msaada wa chakula kuanzia mwezi ujao.

Hata hivyo tayari Serikali imeanza kugawa chakula cha msaada kwa ushirikiano na mpango wa chakula duniani WFP kufuatia ukame ulioathiri mazao katika kipindi cha msimu uliopita.

Comments are closed.