ETHIOPIA YATANGAZA KUYAKABILI MAKUNDI YANAYOHUJUMU AMANI

ETHIOPIA YATANGAZA KUYAKABILI MAKUNDI YANAYOHUJUMU AMANI

Like
250
0
Thursday, 17 December 2015
Global News

WAZIRI MKUU wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amesema serikali yake itakabiliana vikali na makundi yanayohujumu amani baada ya watu kadha kuuawa kwenye maandamano eneo la Oromia.

Serikali inasema watu watano wameuawa kwenye makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama lakini makundi ya upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu yanasema idadi ya waliofariki inakaribia 40.

Akihutubu kupitia runinga ya taifa ya Ethiopia, Bw Desalegn amesema umma pia una jukumu la kutekeleza katika kukabiliana na makundi hayo.

 

 

Comments are closed.