EU YATANGAZA AZMA KUIWEKEA VIKWAZO BURUNDI

EU YATANGAZA AZMA KUIWEKEA VIKWAZO BURUNDI

Like
188
0
Friday, 24 July 2015
Global News

HUKU raia nchini Burundi wakisubiri kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi wa rais na pia kufanyika uchaguzi wa baraza la Seneti leo, Umoja wa Ulaya umetangaza azma ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo ndogo ya Afrika Mashariki.

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, amesema Umoja huo uko tayari kuwawekea vikwazo wale ambao vitendo vyao vilisababisha kutokea kwa ghasia, ukandamizaji, na uvunjwaji wa haki za binaadamu na pia kukwamisha upatikanaji wa suluhisho la kisiasa.

Miongoni mwa wanaotazamiwa kukumbwa na vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya, ni maafisa sita wa serikali, ambao mali zao zitazuiliwa na kuwekewa marufuku ya kusafiri.

Comments are closed.