EURO: CROATIA YAICHAPA HISPANIA 2 – 1

EURO: CROATIA YAICHAPA HISPANIA 2 – 1

Like
373
0
Wednesday, 22 June 2016
Slider

Timu ya Croatia imeichapa Hispania jumla ya magoli 2 – 1 katika mchezo wa kusisimua wa kundi D wa michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya Euro inayochezwa huko Ufaransa.

Hata hivyo timu zote Croatia na Hispania zimesonga mbele katika hatua ya 16 kutokana na kushika nafasi mbili za juu za kundi D.

Katika mechi nyingine ya kundi D iliyochezwa sambamba na hiyo Uturuki imeadhibu Jamuhuri ya Czech kwa jumla ya magoli 2 – 0.

Pamoja na ushindi huo timu zote mbili zimetolewa.

Tayari timu kumi na mbili zimeshafuzu katika hatua ya 16 ambazo ni kama ifuatayo:

Kundi A: Ufaransa na Uswis

Kundi B: Wales na England

Kundi C: Ujerumani and Poland

Kundi D: Uhispania and Croatia

Kundi E: Italy

Kundi F: Hungary

Nyingine zilizofuzu ni Ireland ya Kaskazini ambayo imesonga mbele kwa kushika nafasi ya tatu bora (best looser) kwenye kundi C na Slovakia ambayo nayo imeshika nafasi ya tatu bora kwenye kundi B.

Comments are closed.