EWURA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME IFIKAPO MACHI MOSI MWAKA HUU

EWURA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME IFIKAPO MACHI MOSI MWAKA HUU

Like
253
0
Friday, 13 February 2015
Local News

KUFUATIA agizo lililotolewa na Waziri wa Nishati na Madini hivi karibuni, Mheshimiwa George Simbachawene la kuitaka Mamlaka ya udhibi wa Nishati na Mafuta- EWURA kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za Umeme wa Tanesco, Mamlaka hiyo imetoa tamko la kupunguza gharama za umeme ifikapo Machi mosi mwaka huu.

Tamko hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam, na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi wakati akiongeza na wandishi wa habari ambapo amesema kwa wateja wenye matumizi ya kawaida, bei ya Umeme itashuka kutoka shilingi 306 kwa uniti hadi shilingi 298 kwa uniti sawa na punguzo la shilingi nane.

Ngamlagosi amesema Mfumko wa bei kwa mwaka 2014 ulilazimu kuongeza mahitaji ya pato la Tanesco kwa shilingi bilioni 17.

 

 

Comments are closed.