FA YAMUONYA VAN GAAL

FA YAMUONYA VAN GAAL

Like
212
0
Thursday, 19 February 2015
Slider

 

Meneja wa timu ya Manchester United Louis van Gaal amepewa onyo na shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza kufuatia kauli alizozitoa kuzungumzia matokeo ya mechi kati ya timu yake na Cambridge United kwenye ligi ya Uingereza ambapo mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya bila kufungana mwezi uliopita.

Van Gaal alielekezea lawama zake kwenye Nyanja zote za mechi hiyo kwamba zilikuwa ni dhidi ya timu yake na kuwalaumu waamuzi wa mchezo pia.

FA imetoa onyo hilo mara baada ya Tume Huru ya Udhibiti kukutana tarehe 18 ya mwezi huu wa pili na kufikia maamuzi hayo yakumpa onyo baada ya kumkuta na hatia ya kukiuka sheria za mahusiano ya shirikisho hilo na vyombo vya habari.

Aidha Van gaal kwa upande wake alionyesha kushangazwa na mashtka hayo na kuapa kushinda na maamuzi hayo ya FA

“Kiukweli nimekatihwa tamaa” alisema Van Gaal raia wa Uholanzi alijiunga na klabu hiyo mwezi wa saba

“Kwa takribani miaka 30 nimekuwa mwalimu na meneja pia ila sijawahi kushakiwa, mpaka sasa sidhani kama kuna kitu kibaya nilichokisema. ” aliongeza Van Gaal

Comments are closed.