FA YAPANGA KUANZA MAZUNGUMZO NA ROY HODGISON

FA YAPANGA KUANZA MAZUNGUMZO NA ROY HODGISON

Like
284
0
Thursday, 26 March 2015
Slider

Mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini Uingereza Greg Dyke ameonyesha dhamira yakutaka kuanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba bosi wa kikosi cha England Roy Hodgson kwa mwaka ujao.

Hodgson mwenye umri wa miaka 67 alirithi mikoba ya Fabio Capello mwaka 2012 na kuanza kukinoa kikosi hicho ambacho kwa sasa ndio kinara wa European Championship kwenye hatua za makundi kufuatia ushindi wa michezo yake mine ya awali

Mkataba wa meneja huyu kwa sasa unaelekea mwishoni kwenye michuano ya Euro 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa

Mwneykiti wa shirikisho la soka bwana Dyke ameongeza kuwa wapo kwenye mahusiano mazuri na meneja huyo na wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara lakini bado hawajapata nafasi ya kuzungumzia mkataba wake

Dyke ameeleza kuwa hivi karibuni wataingia kwenye mazungumzo na Roy ili kuhakikisha anabaki kuwa meneja wa kikosi hicho

 

Roy ambae pia aliwahi kuwa meneja wa Switzerland mwaka 1992 hadi 1995 alifanikiwa kutengeza kikosi imara cha England na kuipeleka hatua ya robo fainali za michuanon ya Euro mwa 2012 pia kikosi hicho kilikuwa na historia ya kutoingilika kirahisi katika michuano ya kombe la dunia

 

Comments are closed.