FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA ZAINGIA UTATA KUFUATIA KUENEA KWA EBOLA

FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA ZAINGIA UTATA KUFUATIA KUENEA KWA EBOLA

Like
398
0
Friday, 17 October 2014
Slider

Kuenea kwa ugonjwa wa Ebola umefanya fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kuwa mashakani.

Fainali hizo zimepangwa kufanyika nchini Moroco kuanzia Januari 17 lakini nchi hiyo iliwaeleza waandaji wa mashindano hayo kwamba wangependa kusogeza mbele mashandano hayo.

Serikali ya Moroco imekuwa na wasi wasi maambukizo ya virusi vya ebola kutoka nchi za magharibi mwa Afrika.

Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF linatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho mwezi novemba kama nitasogeza mbele mashindano hayo au la japo limekuwa likisisitiza kuwa mashindano hayo yatafanyika kama kawaida

Wakati huo huo kumekuwa na taarifa kuwa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limeizungumzia nchi za Ghana na Afrika kusisni ili kama zinaweza kukubali kuwa fainali hizo.

DONDOO ZA LIGI KUU UINGEREZA

EPL_Logo

Baada ya ligi mbalimbali duniani kusimama kwa muda ili kupisha mechi za timu za taifa, hekaheka za ligi hizo zinataraji kuendelea tena kesho.

Huko England nyasi za viwanja kadhaa zitakuwa matatani pale timu mbalimbali zitakaposhuka dimbani.

Katika uwanja wa Etihad wenyeji Manchester City watajitupa dimbani kuwakaribisha Tottenham katika mechi itakayotangazwa moja kwa moja na Idha ya Kiswahili ya BBC kuanzia saa saa nane na nusu kwa saa Afrika Mashiriki.

Mechi nyingine zitakazochezwa hiyo kesho ni kati ya Arsenal watakapowakaribisha Hull City, Burnley itapepetana West Ham, Crystal Palace watawakaribisha Chelsea, huku Everton watakuwa nyumbani kumenyana na Aston Villa.

Nayo Newcastle watavaana na Leicester City wakati Southampton itakuwa nyumbani kukwaana na Surnderland.

Siku ya Jumapili Liverpool watakuwa ugenini dhidi ya QPR nayo Stocke City watacheza dhidi ya Swansea City.

 

Comments are closed.