FAMILIA ILIYOTELEKEZWA YAPATIWA MAKAZI YA MUDA NYAMAGANA, MWANZA

FAMILIA ILIYOTELEKEZWA YAPATIWA MAKAZI YA MUDA NYAMAGANA, MWANZA

Like
293
0
Friday, 17 July 2015
Local News

FAMILIA yenye watoto saba  iliyotelekezwa katika mtaa wa Igelegele wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza imepewa makazi ya muda na balozi wa mtaa huo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.

Akizungumza na kituo hiki mmoja wa mtoto wa familia hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Grece  amesema  makazi hayo ya muda yamewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanzo walikuwa wakilala nje na hawakuwa na chakula.

Hata hivyo amesema kuwa kwa upande wa masomo  ameathirika kwa kiasi kikubwa kwani toka shule imefunguliwa  hajahudhulia masomo kutokana na kukosa sare za shule.

Comments are closed.