FBI HUENDA WAKAFUNGUA SIMU YA MUUAJI

FBI HUENDA WAKAFUNGUA SIMU YA MUUAJI

Like
275
0
Tuesday, 22 March 2016
Global News

IDARA ya Haki ya Marekani imesema huenda shirika la upelelezi la FBI limegundua njia ya kufungua simu ya mkononi ya muuaji Syed Rizwan Farook aliyewapiga risasi watu eneo la San Bernardino.

Idara hiyo imeiomba mahakama kuahirisha kusikilizwa kwa kesi kati ya shirika hilo dhidi ya kampuni ya utengenezaji wa simu, Apple.ya iPhone

Idara hiyo imekuwa ikiishawishi mahakama ilazimishe Apple kufungua simu ya Farook, ambaye yeye na mkewe wanatuhumiwa kufanya shambulizi la bunduki na kuwaua zaidi ya watu 14 katika jimbo la California mwezi Desemba mwaka jana.

BBCt

Syed Farook aliwapiga risasi watu San Bernardino

Comments are closed.